1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Septemba 11, uhuru na hofu nchini Iraq: Wasifu wa Aqeel Lazim, daktari wa Iraq

8 Agosti 2011

Vita vya Iraq vya mwaka 2003 ni matokeo muhimu kabisa ya mashambulizi ya 9/11. Muiraki mmoja anakumbuka vipi furaha ya hapo mwanzoni kuhusu Saddam aliepinduliwa, ilivyogeuka kuwa hofu kwa sababu ya matumizi ya nguvu.

https://p.dw.com/p/ReBT
Nur für Projekt 9/11: Porträt Aqeel Ibrahim Lazim (Irak)
Aqeel Ibrahim LazimPicha: DW

Aqeel Ibrahim Lazim alipata habari za mashambulio ya Septemba 11 alipokuwa katikati ya matayarisho ya harusi yake. Daktari huyo wa meno kutoka Basra, aliyemaliza masomo yake katika Chuo Kikuu, alikuwa akishauriana na mchumba wake kuhusu matayarisho ya sherehe za harusi yao.

Alipotupia jicho televisheni iliyokuwepo chumbani, aliona majengo yaliyoshika moto na binadamu wanaokufa - picha ya ukatili kutoka nchi ya mbali ambayo hajawahi kutembelea na, kwa mujibu wa propaganda ya serikali ya Iraq, iliyochukuliwa kama ni adui mkubwa. Pole pole akatambua kuwa anachokiona kwenye televisheni ni tukio halisi na wala sio filamu ya kikatili.

Miaka 10 baada ya Septemba 11

Bild 2: Motiv: Aqeel Ibrahim Lazim, mit Foto 9/11, Basra/Irak, März 2011 Copyright: Ahmed Mohamed Mansour für DW, März 2011 Text Bildergalerie: „Ich kann nur schwer beschreiben, was ich damals empfunden habe“, sagt der Iraker zehn Jahre später rückblickend. „Es war eine Mischung aus Staunen, Mitleid und Schock.“ ***Achtung: Bild darf nur im Zusammenhang mit der Bildergalerie "Irak 9/11 verwendet werden.***
"Nilifikiri huu ni ufunuo."Picha: DW

Sasa miaka 10 baada ya mashambulio ya Septemba 11, Lazim anasema ni vigumu sana kueleza kile alichohisi wakati huo. Ni mchanganyiko wa mshangao, huruma na mshtuko. Alidhani kuwa ule ulikuwa mwisho wa dunia, mwisho wa utamaduni wa binadamu.

Wakati huo, Lazim hakujua kuwa mashambulio yaliyotokea Marekani yasingelivuruga tu maandalizi ya harusi yake, bali pia yangeliitumbukiza nchi yake katika vita vingine na dikteta Saddam Hussein angeling’olewa madarakani. Mashambulio hayo yalimghadhibisha na kumtia wasiwasi pia. Kwani ni mashambulio yaliyofanywa na raia wa kawaida. "Wakati wa kuona huruma, mtu haulizi wahanga ni kutoka wapi au ni raia wa nchi gani", anasimulia Lazim ambaye sasa ana umri wa miaka 35. Anasema alisikitishwa sana na vifo vya watu hao. Lakini hisia hiyo ya huruma haikuwa ya kawaida, kwani waliohusika na mashambulio hayo, walijitambulisha waziwazi kuwa ni Waislamu.

Ilishambuliwa Marekani, ikaumia Iraq

Bild 10: Motiv: Aqeel Ibrahim Lazim in seiner Zahnarztpraxis, Basra/Irak, März 2011 Copyright: Ahmed Mohamed Mansour für DW, März 2011 Text Bildergalerie: Vom Sturz Saddam Hussains hat Aqeel Ibrahim Lazim allerdings profitiert: Eine eigene Zahnarztpraxis und eine Karriere als Universitätsdozent wären für ihn unter dem früheren Regime kaum möglich gewesen. ***Achtung: Bild darf nur im Zusammenhang mit der Bildergalerie "Irak 9/11 verwendet werden.***
Hali ya Usalama Basra bado ni tatizoPicha: DW

Je, usiku huo serikali ilijua kwa umbali gani ugaidi uliofanywa na al-Qaida utaiathiri Iraq? Lazim anasema kuwa usiku wa kuamkia Septemba 12, alihisi kuwa kulikuwepo wasiwasi mkubwa upande wa serikali. Anakumbuka kuwa ghafla, vikosi vya usalama na wafuasi wa chama tawala cha Baath, walionekana mitaani wakibeba silaha. Mtu angedhania kuwa hata Iraq ilikuwa hatarini kufanyiwa mashambulio kama hayo.

Ikazidi kudhihirika kuwa kufuatia mashambulio ya Septemba 11, hata Iraq ilikuwa ikikabiliwa na kitisho cha kutumbukia katika vita vingine. Saddam Hussein alituhumiwa na Marekani kumiliki silaha za maangamizi na hata kuwa na mafungamano na mtandao wa al-Qaida. Baadaye ikadhihirika kuwa tuhuma zote mbili hazikuwa sahihi, lakini kwa Wairaki hiyo ilidhihirisha kuwa mapambano yalikuwa njiani. Lazim anasema, hasahau hotuba moja maarufu ya rais wa wakati huo nchini Marekani. Bush, aliyaambia mataifa makuu kote duniani: "Ama mpo na sisi au mpo dhidi yetu."

Vita vipya vilizuka Machi 19 mwaka 2003. Lazim anakumbuka vizuri akiwa na hisia mbili tofauti. Anasema, miongoni mwa Wairaqi wenzake, wengi walipinga uvamizi wa nchi yao. Wakati huo huo, wote walitaka kumuona Saddam Hussein akipinduliwa. Na hilo lilitokea siku 22 baadaye na wananchi wengi walisherehekea tukio hilo. Lazim anasema, hata hivyo, ilisikitisha kuona miji yao ikikaliwa na vikosi vya kigeni.

Baina ya uhuru, machafuko na hofu

Bild 12: Motiv: Aqeel Ibrahim Lazim, zu Fuß gehend mit seinen Kindern Sarah und Mohammed, Basra/Irak, März 2011 Copyright: Ahmed Mohamed Mansour für DW, März 2011 Text Bildergalerie: Aus Angst vor Autobomben, Morden und Entführungen begleitet Lazim seine beiden eigenen Kinder, Sarah und Mohammed, bis heute jeden Tag persönlich in die Schule.
Leo, Aqeel Ibrahim Lazim anafanya kazi kama daktari wa meno, mjini BasraPicha: DW

Kwa upande mwingine, yeye na wenzake walikuwa na uhuru mpya, baada ya Saddam Hussein kung'olewa madarakani. Anasema, ghafla walikuwa na uhuru wa kueleza maoni yao. Hata kikazi, mambo yamemwendea vizuri, kwani daktari huyo wa meno alifungua kliniki yake mwenyewe, jambo ambalo lisingewezekana wakati wa utawala wa Saddam Hussein.

Lakini uhuru huo mpya, umegharimu maisha ya watu wengi. Nchi hiyo ilitumbukia katika janga la machafuko na ugaidi. Wasunni na Washia waliuana, hakuna aliyeweza kujikinga dhidi ya mashambulio au utekajinyara. Lazim anasema huo sio uhuru waliokuwa wakiulilia. Maelfu ya Wairaqi walipoteza maisha yao katika kipindi hicho. Sasa, hali ya mambo imekuwa bora lakini hakuna hata familia moja ya Kiiraqi isiyosikitika kupoteza ndugu au jamaa. Hata Lazim amepata msiba wakati wa machafuko hayo. Binamu yake, Mohammed, alitekwa nyara na watu wasiojulikana mwaka 2006. Familia yake ilimtafuta kote nchini, lakini hakupatikana na baadaye akatangazwa kuwa amefariki dunia. Maiti yake haikupatikana hadi hii leo.

Bild 12: Motiv: Aqeel Ibrahim Lazim, zu Fuß gehend mit seinen Kindern Sarah und Mohammed, Basra/Irak, März 2011 Copyright: Ahmed Mohamed Mansour für DW, März 2011 Text Bildergalerie: Aus Angst vor Autobomben, Morden und Entführungen begleitet Lazim seine beiden eigenen Kinder, Sarah und Mohammed, bis heute jeden Tag persönlich in die Schule.
Lazim huwapeleka watoto wake shule kila siku kutokana na uoga wa mashambuliziPicha: DW

Lazim anapotazama picha za mashambulio ya Septemba 11, basi hufikiria pia jinsi ugaidi unavyowaathiri wale walionusurika. "Hapa Iraq, watoto wengi wasio na hatia yoyote, wanazaliwa katika mazingira ya vita, machafuko na ugaidi. Watoto hawa wameshuhudia mengi na wanaishi kwa woga mkubwa". Anasema Lazim. Hadi leo hulazimika yeye mwenyewe kuamka kila siku asubuhi kuwapeleka skuli watoto wake wawili, Mohamed na Sara. Sababu ni kuwa anahofia usalama wa watoto wake.

Mwandishi: Munaf Al Saidy/ZPR

Tafsiri: Prema Martin