SEOUL:Korea Kusini kuongeza muda wa jeshi lake kubakia Iraq
23 Oktoba 2007Matangazo
Korea kusini imesema inapanga kuongeza muda wa mwaka mmoja kubakia Iraq wanajeshi wake.Hata hivyo rais wa nchi hiyo Roh Mo Hyun amesema itapunguza wanajeshi hao hadi kufikia 600.Kwa sasa Korea kusini inawanajeshi kiasi 1200 katika eneo lililona utulivu linalokaliwa na wakurdi huko kaskazini mwa Iraq.Korea Kusini iliwahi kuwa na wanajeshi wengi zaidi nchini humo baada ya Marekani na Uingereza lakini imekuwa ikipunguza wanajeshi wake kutokana na mbinyo wa wananchi wakutaka vikosi vya kigeni viondoke nchini humo.