SEOUL: Wanafunzi 1000 wa Korea Kusini wapambana na Polisi
30 Mei 2005Matangazo
Takriban wanafunzi 1000 wa Korea Kusini waliokuwa wakiandamana dhidi ya sera za Marekani kuelekea Korea Kaskazini,wamepambana na polisi wakukabiliana na fujo hapo jana.
Kulingana na habari za polisi wanafunzi wasiopungua 10 wamejeruhiwa na wengine 30 walitiwa ndani lakini baadae waliachiwa huru.
Wanafunzi hao walikuwa wakiandamana kuelekea ngome ya kijeshi ya Marekani kati kati ya mji mkuu wa Korea Kusini ,Seoul .
Maandamano hayo yamekuja wakati jumuiya ya Ulaya imeamua kurejesha Korea Kaskazini katika meza ya wanachama sita ya mazungumzo juu ya kumaliza mpango wake wa kutengeneza silaha za Nuklear.
Mazungumzo kati ya nchi za Marekani,China,Japan,Russia ,Korea Kusini Na Kaskazini yamemaliza zaidi ya mwaka mmoja.