SEOUL : Wakaguzi wa nuklea kuwekwa Korea Kaskazini
8 Julai 2007Shirika la habari la Korea Yonhap linaripoti kwamba shirika la masuala ya nuklea la Umoja wa Mataifa linapanga kuwaweka wafanyakazi wawili nchini Korea Kaskazini kuanzia wiki ijayo kuyakinisha hatua ya serikali ya Korea Kaskazini kutokomeza silaha zake za nuklea.
Kwa mujibu wa Yonhap mwishoni mwa juma lijalo timu ya wakaguzi wanane wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomu watakwenda nchini humo kuimarisha timu ya wakaguzi wengine walioruhusiwa kuingia nchini Korea Kaskazini mwezi uliopita.
Wawili kati ya wakaguzi hao wataendelea kubakia nchini humo katika kipindi kisichokuwa na kikomo kufuatilia hatua ya serikali ya nchi hiyo katika kutimiza makubaliano yaliofikiwa mwezi wa Februari kungowa mitambo yake ya nuklea ili badala yake iweze kupatiwa msaada pamoja na nishati.