SEOUL: Vikosi vya Korea ya Kusini kuondoka Afghanistan
22 Julai 2007Matangazo
Korea ya Kusini,imeanza kufanya matayarisho ya kuviondosha vikosi vyake kutoka Afghanistan ifikapo mwisho wa mwaka huu,kama ilivyopangwa hapo awali.Maafisa hii leo wamethibitisha hatua hiyo,huku ikidaiwa kuwa Wataliban wamesema, mahabusu 23 wa Korea ya Kusini wataachiliwa huru kwa kubadilishana na wapiganaji wa Taliban waliozuiliwa katika jela.Wanamgambo wa Taliban, wameonya kuwa watawaua raia wa Korea ya Kusini ikiwa hadi saa moja jioni,Jumapili ya leo, serikali ya Seoul haitokubali kubadilishana mahabusu na wafungwa.
Wakati huo huo tume ya Korea ya Kusini,imewasili nchini Afghanistan,kujaribu kupata uhuru wa mahabusu waliozuiliwa na Taliban.