1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Seoul. Mwanajeshi awauwa wenzake baada ya kunyanyaswa.

19 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF1v

Mwanajeshi mmoja wa Korea ya kusini ambaye anaripotiwa kuwa alifanyiwa vitendo vya uonevu na maafisa wa ngazi za juu amewauwa wanajeshi wenzake wanane, na kuwajeruhi wengine wawili. Mwanajeshi huyo mwenye umri wa miaka 22 alitupa bomu la kutupwa kwa mkono eneo la jeshi wakati wengine wakiwa wamelala, na kisha kuwafyatulia risasi.

Tukio hilo lilitokea katika eneo la lindo huko Yonchon, umbali mdogo kutoka katika eneo linalolindwa la mpaka na Korea ya kaskazini. Wizara ya ulinzi ya Korea ya kusini imesema kuwa mwanajeshi huyo ambaye hana cheo amekuwa akitukanwa na kufanyiwa ukatili na viongozi wa ngazi za juu. Kamanda wa kikosi alichokuwamo mwanajeshi huyo ni miongini mwa wale waliouwawa katika shambulio hilo.