1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Seoul: Mazungumzo ya programu ya Kkinyukliya ya Korea kaskazini yataanza karibuni

12 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEFc

Korea Kusini imeamuwa kuipa Korea kaskazini msaada wa tani laki tano za mchele baada ya Korea Kaskazini kuamua kurejea tena katika mazungumzo baina ya nchi sita kuhusu programu yake ya kinyukliya. Nchi mbili za Korea pia zimekubaliana kuziunganisha tena njia zao za reli kupitia mpaka wao wa pamoja.

Akiitembelea Japan, waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Bibi Condoleezza Rice, ameitaka Korea Kaskazini ifanye uamuzi muhimu wa kuachana na silaha zake za kinyukliya. Idara za ujasusi za Marekani zinakisia kwamba Korea Kaskazini ina mabomu manane ya kinyukliya. Kwa upande mwengine, Uchina imemtuma mwakilishi wake maalum, Tang Jiaxuan, hadi Korea kaskazini, kuyatayarisha mashauriano hayo ya nchi sita. Mazungumzo yanatazamiwa kuanza tena July25 baada ya kusita kwa miezi 13.

Viongozi wa nchi nane tajiri duniani, katika mkutano wao wa kilele huko Scotland wiki iliopita, walisema wana wasiwasi sana juu ya mpango wa kinyukliya wa Korea Kaskazini.