Seoul. Mazungumzo ya Korea mbili kuhusu suala la Kinuklia la Korea ya kaskazini yakwama.
17 Mei 2005Matangazo
Mazungumzo kati ya Korea mbili yalikwama leo kuhusiana na suala la kinuklia baada ya Korea ya kaskazini kuweka kando pendekezo kutoka Korea ya kusini la kutaka kuanzishwa tena mazungumzo ya nchi sita.
Taarifa zinasema kuwa mipango ya chakula cha pamoja ilivunjika kufuatia kikao cha asubuhi ambacho kilimwacha kiongozi wa ujumbe wa Korea ya kusini , waziri mdogo wa masuala ya muungano Rhee Bong-Jo akiwa amekasirishwa na uamuzi wa Korea ya kaskazini. Bwana Rhee amesema kuwa juhudi zimefanyika kupata msimamo wa pamoja, lakini majadiliano zaidi yanatakiwa kuhusiana na suala la kinuklia.