1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SEOUL : Marekani kutosubiri milele mazungumzo ya Korea Kaskazini

20 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFVB

Marekani na mataifa makubwa ya Asia kuzidisha jitihada za kuanzisha tena mazungumzo yaliokwama ya nchi sita juu ya suala la Korea Kaskazini kutengeneza silaha za nuklea lakini kuchelewa kuanza kwa mazungumzo hayo hakuwezi kusubiriwa milele.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleezza Rice amewaambia waandishi wa habari kufuatia mkutano wake na viongozi wa Korea Kusini kwamba mawasiliano ya moja kwa moja kati ya Marekani na maafisa wa Korea Kaskazini yanawezekana kwenye mazungumzo ya nchi hizo sita lakini sio nje ya mpangilio huo.

Serikali ya Korea Kaskazini imekuwa ikidai kuwepo kwa majadiliano kati ya nchi hizo mbili na kuweka masharti mengine ya kurudi kwenye mazungumzo hayo ambayo yanazijumuisha China, Japani,nchi mbili za Korea,Russia na Marekani.

Rice amesema Marekani imejifunga kulitatuwa suala hilo kidiplomasia lakini haliwezi kuachiliwa kuendelea milele.

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani tayari amewasili nchini China leo hii kwa ziara ya siku mbili ikiwa ni mkondo wa mwisho wa ziara ya mataifa sita barani Asia.