SEOUL: Korea ya Kusini yaonya Korea Kaskazini huenda ifanye jaribio la nyuklia wikendi hii
6 Oktoba 2006Korea ya kusini imeonya kwamba Korea ya Kaskazini huenda ifanye jabio la kinyuklia mwishoni mwa juma. Kiongozi wa Korea Kaskzini Kim Jong Il amewatahadharisha viongozi wa ngazi ya juu wa jeshi lake na amewataka waviandae vikosi vyao.
Rais wa Korea Kusini, Roh Moo-Hyun amekatiza likizo yake na kurudi mjini Seoul ili kuushughulikia mzozo huo. Wakati huo huo baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limefikia makubaliano ya kuionya Korea Kaskazini iwachane na jaribo lake la nyuklia na irudi kwenye mazungumzo ya mataifa sita. Makubaliano hayo yanasubiri kuidhinishwa na wanachama wa baraza hilo.
Akizungumza juu ya tisho la Korea Kaskazini, naibu waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani, Christopher Hill amesema,
´Kwa Korea Kaskazini kuripua sihala ya nyuklia mahala padogo ambako watu milioni 70 wanaishi, na hata kwa sababu za kimazingira ni kitendo kiovu cha ukatili. Lakini kusema wazi, kisiasa tuna makubaliano ya mataifa sita. Kuna mengi kuhusu Korea Kaskazini, kwa hiyo unatakiwa kujiuliza kwa nini wafanye hivyo?
Ripoti zilizotolewa na vyombo vya habari zinasema jaribio la nyuklia huenda lifanywe kesho kutwa Jumapili, siku ya kuadhimisha kuteuliwa kwa Kim kama kiongozi wa chama cha Korean Workers Party mnamo mwaka wa 1997.