1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SEOUL Korea Kazkazini yataka eneo la Korea lisiwe na silaha za kinuklia

22 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF1F

Korea kazkazini inataka eneo la Korea liwe huru kutokana na silaha za kinuklia. Msemaji wa Korea Kusini, Kim Chun Shick, alimnukulu kiongozi wa wajumbe wa Korea Kazkazini, Kwon Ho-Ung, akisema nchi yake haingehitaji silaha za kinuklia kama Marekani ingekuwa rafiki wake.

Kwon alikuwa akizungumza katika kikao cha baraza la mawaziri kutoka mataifa hayo mawili kinachoendelea mjini Seoul hadi Ijumaa wiki hii. Mazungumzo ya mkutano huo yanatuwama juu ya ushirikiano kati ya Korea Kazkazini na Korea Kusini, lakini kiongozi wa ujumbe wa Korea Kusini, Chung Dong-Yong, amesisitiza kwamba ni lazima swala la mzozo wa nuklia lijadiliwe.