SEOUL: Huduma za treni baada ya nusu karne
16 Novemba 2007Matangazo
Korea ya Kaskazini na ya Kusini zimekubaliana kuanzisha huduma za treni kati ya nchi hizo mbili kuanzia mwezi ujao.Kwa hivyo,kwa mara ya kwanza tangu zaidi ya nusu karne,kutakauwepo usafiri wa treni kati ya Korea hizo mbili.Mwanzoni huduma hizo za treni zitahusika na usafirishaji wa mizigo tu,hadi kwenye kiwanda kinachosimamiwa na nchi hizo mbili katika mji wa mpakani wa Kaesong, nchini Korea Kaskazini.
Makubaliano yaliyopatikana leo Ijumaa yanatoa mwito pia kwa Korea Kusini mwakani,kuanza kujenga viwanda vya kutengenezea meli nchini Korea Kaskazini na pia kufanyia ukarabati barabara kuu na njia ya reli katika nchi hiyo masikini.