1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SEOUL Condoleeza Rice ana matuamini ya kufikiwa makubalinao juu mpango wa nuklia wa Korea Kazkazini

14 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEuh

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Bi Condoleezza Rice ana matumaini ya kufikiwa makubaliano katika mazungumzo kuhusu mpango wa nuklia wa Korea Kazini. Amesema Korea Kazkazini huenda ikakubali kufutilia mbali mpango wake wa nuklia kwa kupewa msaada wa umeme. Korea Kusini imesema imejitolea kuipatia Korea Kazkazini umeme na msaada wa chakula.

Baada ya kukataa kushiriki katika mazungumzo kwa mwaka mmoja, Korea Kazkaini ilikubali kurudi kwenye mazungumzo hayo mwishoni mwa juma lililopita. Mataifa mengine yanayoshiriki katika mkutano huo ni China, Marekani, Korea Kusini, Japan na Russia.