1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Seneti Nigeria yabadili sheria ya matokeo ya uchaguzi

13 Oktoba 2021

Baraza la Seneti la Nigeria Jumanne limepiga kura kuifanyia marekebisho sheria ili kuiruhusu tume ya uchaguzi, kuamua juu ya uhamishaji wa kielektroniki wa matokeo ya uchaguzi kuelekea uchaguzi wa rais 2023.

https://p.dw.com/p/41cPQ
Nigeria Politik l Senat
Picha: Getty Images/AFP/K. Sulaimon

Ni suala tete nchini Nigeria, ambako mara nyingi uchaguzi hukumbwa na madai ya udanganyifu na mapingamizi ya mahakamani, tangu nchi hiyo iliporejea kwenye utawala wa kiraia mwaka 1999.

Maseneta wameidhinisha mabadiliko ya sheria ya uchaguzi mnamo mwezi Julai, lakini chama tawala cha APC na wabunge wa upinzani walitofautiana juu ya iwapo tume huru ya uchaguzi inaweza kuamua juu ya uhamishaji wa kielektroniki wa matokeo.

Tume yauchaguzi ilikosolewa baada ya kuchaguliwa upya kwa rais Muhammadu Buhari mwaka 2019, kuhusiana na madai kuwa kura hiyo haikuwa huru na ya haki katika taifa hilo la wakaazi milioni 210.