Seneti imepinga mswada wa deni Marekani
30 Julai 2011Hii ni baada ya baraza la wawakilishi nchini Marekani limeidhinisha pendekezo la chama cha Republican, kupandisha kiwango cha ukopaji cha nchi hiyo katika awamu mbili, kupitia kura 218 dhidi ya 210.
Baadhi ya wanachama wa Republican walijiunga na wale wa Democratic kupinga hatua hiyo ya wabunge wenzao.
Wasiwasi ulizidi kufuatia kuwadia siku ya Ijumanne ambayo wizara ya fedha ya Marekani inasema ndio siku ya mwisho kuwa na akiba ya kutosha ili kuweza kutekeleza wajibu wake wa kuwalipa wamiliki wa hisa za serikali pamoja na wastaafu, maskini, na wale wanaohitaji huduma za afya.
Spika wa bunge John Boehner aliahirisha kura hiyo kwa siku mbili, akibishana na wanachama wenzake katika jitahada ya kuwashawishi kuunga mkono mpango huo.
Mwandishi: Maryam, Abdalla/Dpae/Rtre
Mhariri:Martin, Prema