UchumiSenegal
Senegal yaanza uzalishaji wake wa kwanza wa mafuta
11 Juni 2024Matangazo
Kumekuwa na matumaini kuwa uzalishaji wa mafuta na gesi utaongeza mapato ya mabilioni ya dola nchini humo na kuchangia katika kuboresha uchumi wa Senegal.
Mradi huo unalenga kuzalisha mapipa 100,000 ya mafuta kwa siku. Sehemu kunakochimbwa mafuta pia kunapatikana gesi asilia.
Kampuni ya Woodside inamiliki asilimia 82 ya hisa katika mradi huo huku sehemu iliyobaki ikishikiliwa na kampuni ya nishati Petrosen, inayomilikiwa na serikali.
Ugunduzi wa maeneo ya mafuta na gesi mwaka 2014 uliibua matumaini makubwa kwa nchi hiyo inayoendelea, huku kampuni ya taifa ya nishati ikikadiria kuwa sekta hiyo itazalisha zaidi ya dola bilioni 1 kwa mwaka katika kipindi cha miongo mitatu ijayo.