1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Senegal Vs Mali: Mafunzo kwa demokrasia ya Afrika?

1 Aprili 2012
https://p.dw.com/p/14VwY
Furaha ya ushindi Senegal.
Furaha ya ushindi Senegal.Picha: REUTERS

Senegal imefanya mabadiliko ya utawala kwa njia ya amani kwa mara nyengine tena katika historia, ambapo Rais Abdoulaye Wade amekubali kupoteza uchaguzi kwa kiongozi wa upinzani, Macky Sall, na hivyo kuinusuru na maafa.

Lakini wakati Senegal ikiingia awamu nyengine ya utawala wa kidemokrasia, nchi jirani ya Mali imefanya mapinduzi ya kijeshi kumuondoa kiongozi wa kijeshi aliyegeuka kuwa kiongozi wa kiraia, Amadou Toumani Toure, kwa madai ya kiongozi huyo kushindwa kuwadhibiti waasi wa Toureg wa kaskazini mwa nchi hiyo. Je, ni mafunzo gani Senegal inatoa kwa Afrika? Na je, Mali na Senegal ni taswira mbili za eneo moja zinazokinzana?

Sikiliza kipindi cha Maoni kutoka Deutsche Welle, ambapo Mohammed Khelef amewaalika kujadili mada hii Salim Himidi kutoka Paris, Ufaransa; Ahmed Rajab akiwa Nairobi, Kenya; Profesa Tom Namwamba kutoka Chuo Kikuu cha Kenyatta, Kenya; na Ayoub Rioba kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania.

Kusikiliza tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mtayarishaji: Mohammed Khelef
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman