1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SENEGAL IN M IADI NA KAMERUN FEBRUARI 9: RUDI VÖLLER KUWA TENA MKURUGENZI WA BAYER LEVERKUSEN NA KIPCHOGE KEINO LEO ASHEREHEKEA SIKU YA KUZALIWA (MIAKA 65)

17 Januari 2005
https://p.dw.com/p/CHZZ

-SIMBA WA NYIKA KAMERUN KUPAMBANA NA SENEGAL FEBRUAI 9 HUKO UFARANSA

-RUDI VÖLLER ARUDI BAYER LEVERKUSEN KAMA MKURUGENZI WA DIMBA

NA KIPCHOGE KEINO ‘MFALME WA MBIO BARANI AFRIKA’ ASHEREHEKEA MIAKA 65 YA SIKU YA KUZALIWA

Tuanze na Dundesliga inayorudi uwanjani wiki ijayo kufuatia likizo ya X-masi na mwaka mpya :

Mabingwa wa Ujerumani Werder Bremen wanakabili uwezekano wa kumpoteza mshambulizi wao mpya waliomuazima majuzi kutoka klabu ya Midtyland ya Danmark,Mmisri Mohamed Zidan.Chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 23 ameumia baada ya kugongana na mchezaji mwenzake wa kiungo Raphael Wicky na akapelekwa hospitali kumurikwa goti lake.Anatazamiwa Zidan kuwa nje ya chaki ya uwanja kwa muda wa wiki 6.

Mmisri huyo aliazimwa kuimarisha mkuki wa Bremen katika Bundesliga na kombe la klabu bingwa barani Ulaya baada ya Bremen kumuuza Mgiriki Charisteas kwa Ajax Amsterdam.Bremen inafungua dimba la Bundesliga jumamosi ijayo ikiwa na miadi na Schalke 04.

BAYER LEVEKUSEN,inatazamiwa kutangaza kumrejesha mkurugenzi wake wa zamani wa spoti-Rudi Völler.Völler,mwenye umri wa miaka 44, alikua katika madaraka hayo kabla kuchaguliwa kuwa kocha wa Taifa wa Ujerumani.Halafu kufuatia kindumbwendumbwe ilichochezeshwa Ujerumani katika Kombe la ulaya la mataifa kati ya mwaka jana huko Ureno,alijiuzulu na mahala pake akachukua Jürgen Klinsmann.

Taarifa kutoka Dakar, senegal zinasema simba wa Senegal waliosisimua mno katika kombe lililopita la dunia 2002 huko Korea na Japan wana miadi na simba wa nyika hapo februari 9 huko Ufaransa kuoneshan a nani hasa ni simba wa nyika.M kutano huo umetangazwa leo na chama cha mpira cha Senegal.

Changamoto hii ni kuzinoa timu zote mbili kwa changamoto zao za kombe la dunia hapo machi.Kamerun iliitoa Senegal katika changamoto za mikwaju ya penalty ili kutawazwa mabingwa wa Afrika 2002 baada ya zahama yao kubakia suluhu 0:0 hata baada ya kurefushwa muda.

Hebu tujiunge sasa na mwanamichezo wetu Makame Abdullah akituarifu jinsi klabu za Tanzania zinavyojiwinda kwa vikombe vya CAF-shirikisho la dimba la Afrika na iwapo uwanja wa Amani huko visiwani unahimili vishindo vya Kombe hilo ?

Tumalizie KIP KEINO aliepigiwa upatu miaka ya 1970 kama "Mfalme wa mbio barani Afrika".

Mkenya Kip Keino, leo mwenyekiti wa kamati ya Olimpik ya Taifa ya Kenya, anasherehekea siku yake ya kuzaliwa:ametimiza miaka 65.

Kip Keino akielezwa ndie ‘mfalme wa mbio barani Afrika’-King of African Track.Isitoshe,mwenyekiti huyu wa sasa wa Kamati ya olimpik ya taifa ya Kenya, akiitwa ‘Balozi bora kabisa wa Kenya’ nchi z6a n’gambo-kwani amechangia zaidi kuliko mwanariadha yoyote wa Kenya, kuiweka nchi hii katika ramani ya dunia.

Keino,amezaliwa Januari 17,siku kama leo,1940 kutoka kabila la nandi.1957 aliondoka kijini mwake na kujiunga na kikosi cha Polisi mjini Nairobi.Wakuu wake wa spoti huko walisangazwa na ustadi wa chipukizi huyo wa miaka 17 katika kutimka mbio.Na ugunduzi wao huo ukawa chanzo cha maisha maridadi ajabu ya riadha.

Keino alishiriki kwa mara ya kwanza katika michezo ya olimpik ya Tokyo,1964 akamaliza 5 katika finali ya mita 5000.Akapigwa kumbo katika mbio zake hasa za mita 1.500 hata kabla ya finali.

Lakini, miaka 4 baadae katika michezo ya olimpik ya Mexico City, Kip keino aliwasili hasa katika medani ya olimik.Alimtimua nje kwa msaada wa benjamin jipcho,bingwa wa rekodi ya dunia wakati ule muamerika Jimy Ryun na kutwaa medali yake ya kwanza ya dhahabu ya olimpik.

Miaka 4 baadae, alitetea taji lake hilo katika michezo ya olimpik ya munich hapa Ujerumani.Lakini,kinyume na miaka 4 kabla hakuwa na kasi za kumpiku mfinland Vassala Pekka na akaondokea na medali ya fedha.

Lakini kabla ya mbio hizo aliwasangaza wote alipompiku hata BIG BEN-Benjipcho na kutwaa medali yake ya pili ya dhahabu ya olimpik katika mchezo asiotazamiwa-mita 3000 kuruka viunzi.

Kutoka hapo alikwenda katika michezo yake ya mwisho ya bara la Afrika-2nd.All Africa games, mjini Lagos,Nigeria.

Ilikuwa uwanjani Lagos binafsi nilipomuona chipukizi wa tanzania bado si maarufu sana,Philbert Bayi,akimuuzulu kitini 'm‘alme wa mbio barabni Afrika.

Kip keino hakudiriki hata kusubiri michezo hii kumalizika, alifunga safari hadi NY na kufunga mkataba kama muajiriwa kufufua uhasama wake na Muamerika Jimy Ryun.

Baada ya kuwa kocha wa riadha wa Kenya,Kip Keino,leo ni mwenyekiti wa Kamati ya olimp0ik ya Kenya ambayo majuzi tu imetangaza itaania kuamndaa michezo ya kwanza kabisa ya olimpik barani Afrika 2016:

Bila ya shaka Kip keino amechangia mno hadi Kenya kufikia hapo.Tunamtakia heri na maisha marefu zaidi leo Kip keino.