1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sekta ya afya yaathirika pakubwa kutokana na mizozo Ethiopia

26 Novemba 2024

Waziri wa Afya wa Ethiopia Ayele Teshome, amesema mzozo usioisha katika eneo la vita la Amhara nchini Ethiopia umezorotesha mfumo wake wa afya.

https://p.dw.com/p/4nRoW
Wagonjwa wakiwa katika hospitali moja nchini Ethiopia
Wagonjwa wakiwa katika hospitali moja nchini EthiopiaPicha: Million Haileselasie/DW

Waziri wa Afya wa Ethiopia Ayele Teshome, amesema mzozo usioisha katika eneo la vita la Amhara nchini Ethiopia umezorotesha mfumo wake wa afya.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Addis Ababa, Ayele, amesema athari za mzozo huo kwa huduma za afya na binadamu ni mbaya mno.Takriban wafanyakazi wanane wa kutoa misaada waliuawa nchini Ethiopia, sita kati yao waliuliwa huko Amhara.

Ameongeza kusema upatikanaji wa huduma muhimu "umezorota kwa kiasi kikubwa, wanashuhudia viwango vya kutisha vya utapiamlo, hasa miongoni mwa watoto na wanawake walio katika mazingira magumu, akitoa wito wa msaada wa kimataifa.

Upatikanaji wa misaada ya kiutu umekuwa mgumu kutokana na hali ya usalama, hasa utekaji nyara wa mara kwa mara kwa ajili ya kikombozi. Kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kibinadamu la OCHA,