1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Schäuble aagwa katika bunge la Ujerumani

22 Januari 2024

Wanasiasa na viongozi wa ngazi za juu kutoka kada mbalimbali wamekusanyika mjini Berlin kutoa heshima za mwisho kwa mwanasiasa mkongwe aliyewahi kuwa spika wa bunge na waziri wa wizara kadhaa, Wolfgang Schäuble.

https://p.dw.com/p/4bYNq
Wolfgang Schäuble, Berliner Dom
Muili wa waziri wa zamani wa fedha na pia aliyekuwa spika wa bunge la Ujerumani, Wolfgang Schäuble, uliagwa rasmi siku ya Jumatatu (Januari 22) kwenye Bunge la Ujerumani.Picha: Sebastian Gollnow/dpa/picture alliance

Karibu watu 1,500 walishiriki kwenye hafla hiyo iliyoandaliwa kwenye majengo ya bunge la Ujerumani, akiwamo Rais Emmanuel Macron, ambaye pia alisoma wasifu wake.

Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani, Rais wa Shirikisho Frank-Walter Steinmeier na Rais wa Bunge la Ujerumani, Bärbel Bas, pia wanahudhuria shughuli hiyo.

Schäuble aliyenusurika katika jaribio la kuuawa mwaka 1990, aidha alikuwa mbunge wa chama cha kihafidhina cha Christian Democrat kuanzia mwaka 1972 hadi kifo chake.

Tukio hili lilitanguliwa na misa katika Kanisa Kuu la Berlin Cathedral mchana wa Jumatatu (Januari 22).