1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Schröder akutana na Rais wa Ghana

24 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFhY
ACCRA: Akikamilisha ziara yake barani Afrika Kansela Gerhard Schröder wa Ujerumani leo amekutana mjini Accra na Rais John Agyekum Kufuor wa Ghana. Katika sherehe rasmi ya chakula cha usiku hapo jana Rais Kufuor alitoa mwito wa kuondolewa lile pengo la tafauti katika uchumi wa kimataifa kwa sababu hali kama hiyo inaweza kutumiwa kwa shabaha za ugaidi. Hii leo Kansela Schröder atakutana tena na Rais Kufuor kwa madhumuni ya kutiliana saini mkataba wa msamaha wa madeni. Pia Kansela atafungua Kituo cha Kuhakikisha Amani kitakachogharimiwa sehemu kubwa na Ujerumani. Wakati wa ziara yake ya wiki moja barani Afrika, Kansela Gerhard Schröder alizizuru pia Ethiopia, Kenya, Afrika ya Kusini.