1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Schröder aizuru Ghana:

24 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFhS
ACCRA: Akikamilisha ziara yake barani Afrika Kansela Gerhard Schröder wa Ujerumani leo ameahidi kuunga mkono juhudi za amani za nchi za Kiafrika. Bila ya amani watu wa Afrika watanyimwa sehemu yao katika matunda ya mfumo wa kimataifa wa utanda wazi, alisema Kansela Schrödr mjini Accra, mji mkuu wa Ghana ambako alifungua Kituo cha Mafunzo ya Kuhakikisha Harakati za Amani Barani Afrika kinachoitwa kwa jina Kofi Annan, Katibu Mkuu wa UM. Pamoja na Rais John Agyekun Kufuor, Kansela Schröder alisaini mkataba wa kuisamehe Ghana deni la EURO Miliyoni 220. Wakati wa ziara yake ya wiki moja barani Afrika, Kansela Gerhard Schröder alizizuru pia Ethiopia, Kenya, Afrika ya Kusini.