SCHROEDER KUVUTIA BIASHARA:
21 Novemba 2003Matangazo
NEW YORK: Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani yupo mjini New York kwa ziara ya siku mbili.Wakati wa ziara hiyo anakutana na viongozi wa mashirika ya kibiashara ya Kimarekani akijaribu kuwavutia kufanya biashara nchini Ujerumani.Ingawa mzozo kuhusu suala la Iraq ulisababisha mvutano katika uhusiano wa kisiasa,Schroeder amesema uhusiano wa kibiashara kati ya Marekani na Ujerumani ni mzuri mno.Kwa wakati huo huo Schroeder ameihimiza Marekani iheshimu uamuzi wa Shirika la Biashara Duniani WTO,kuwa ushuru uliowekwa na Marekani kwa chuma cha pua kinachoingizwa Marekani ni kinyume na sheria,au ikabiliane na matokeo yake.