1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Scholz, Putin wazungumza kwa mara ya kwanza tangu 2022

15 Novemba 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais wa Urusi Vladimir Putin hii leo.

https://p.dw.com/p/4n3W9
Rais wa Urusi Vladimir Putin  na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz
Rais wa Urusi Vladimir Putin na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz Picha: Kay Nietfeld/Sputnik/AP/dpa/picture alliance

Hii ni mara ya kwanza kwa viongozi hao kuzungumza katika kipindi cha takriban miaka miwili tangu Urusi ilipoanzisha uvamizi kamili nchini Ukraine.

Chanzo cha kuaminika kimeeleza kuwa Scholz amezungumza na Putin kwa muda wa saa moja.  Msemaji wa serikali mjini Berlin amesema katika mazungumzo hayo, Kansela Scholz amemtaka Putin kuondowa wanajeshi wake wote nchini Ukraine.

Kabla ya kuzungumza na Putin, Scholz alikuwa amezungumza kwa simu na Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine na kumuhakikishia uungwaji mkono wa kudumu wa Ujerumani kwa Ukraine.