JamiiMisri
Scholz na Rais wa Misri wazungumzia hali ya mgogoro wa Gaza
29 Januari 2024Matangazo
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Ujerumani, Steffen Seibert, viongozi wote wawili wamekubaliana kwamba ufikishaji wa msaada wa kiutu na mahitaji mengine katika Ukanda wa Gaza unapaswa kuimarishwa.
Kadhalika wamesema raia walioko kwenye eneo hilo la vita kati ya kundi la wanamgambo la Hamas na Israel wanapaswa kulindwa.
Lakini pia katika taarifa iliyotolewa, Kansela Olaf Scholz amesisitiza kwamba Ujerumani inaunga mkono suluhisho la kuweko madola mawili kuupatia ufumbuzi mgogoro huu.
Scholz na Al Sisi imeelezwa kwamba kwa pamoja wamekubaliana kwamba juhudi zinatakiwa kufanyika kuzuia kutanuka kwa vita hivyo.