Scholz: Magharibi yajadili 'dhamana za usalama' kwa Ukraine
2 Machi 2023Matangazo
Scholz ameyasema hayo katika hotuba yake mbele ya bunge la Ujerumani leo na kuongeza kuwa Ujerumani itaendelea kuiunga mkono Kyiv kwa kuipatia silaha.
Wakati akitoa wito kwa Urusi kuondoa wanajeshi wake Ukraine, Scholz ametumia pia hotuba hiyo kuionya China dhidi ya kuipatia Urusi silaha katika vita hivyo.
Kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Ujerumani imeongeza uwekezaji katika jeshi lake na kuvunja uhusiano wa kiuchumi na Urusi na kuweka kando msimamo wake wa kutopeleka silaha katika maeneo yenye migogoro.