1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz kukutana na Xi pembezoni mwa mkutano wa G20

15 Novemba 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz anatarajiwa wiki ijayo kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na rais wa China, Xi Jinping.

https://p.dw.com/p/4n3W5
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz.Picha: Carsten Koall/dpa/picture alliance

Mazungumzo hayo yatafanyika pembezoni mwa mkutano wa kilele wa mataifa yanaoyoongoza kiuchumi duniani G20 utakaofanyika nchini Brazil.

Scholz na Xi watakutana siku ya Jumanne na kujadili vita vya Ukraine na Mashariki ya Kati, uhusiano kati ya China na Ujerumani pamoja na usawa wa kibiashara duniani.

Scholz ambaye alikutana na Xi mara ya mwisho mwezi Aprili mjini Beijing, hakudiriki kutoa maneno makali kwa China kama ilivyofanya Marekani na mataifa mengine ya Ulaya, na badala yake ameonesha nia ya kuwa mshirika muhimu wa Beijing.

Mwaka jana, China ilikuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Ujerumani, taifa lenye uchumi mkubwa zaidi barani Ulaya, ambalo hata hivyo uchumi wake unatarajiwa kushuka kwa mwaka wa pili mfululizo.