1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz aushutumu uongozi wa Iran kwa kupigana na watu wake

22 Februari 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, ameelezea hukumu ya kifo iliyotolewa na mahakama mjini Tehran dhidi ya Mjerumani mwenye uraia pia wa Iran, Jamshid Sharmahd, kuwa "haikubaliki."

https://p.dw.com/p/4NqP2
Protest gegen Hinrichtung im Iran
Picha: Ying Tang/NurPhoto/IMAGO

Katika ukurasa wake wa Twitter, Scholz ameandika "utawala wa Iran unapigana na watu wake wenyewe na kupuuzilia mbali haki za binaadamu.

Amesema wanalaani hukumu hiyo kwa nguvu zote na kutoa wito kwa serikali ya Iran kubatilisha uamuzi huo.

Mapema Jumatano serikali ya Ujerumani pia iliwafukuza wanadiplomasia wawili wa Iran kutokana na kuipinga hukumu ya kifo.

Mahakama ya Walinzi wa Mapinduzi ya Iran imemuhukumu Sharmahd mwenye umri wa miaka 67, kwa tuhuma kadhaa zikiwemo mashambulizi ya kigaidi, tuhuma ambazo haziwezi kuthibitishwa.