1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz aelekea Sweden kwa mazungumzo na viongozi wa Nordic

Saleh Mwanamilongo
13 Mei 2024

Kansela wa Ujerumani, Olaf Sholz, anatarajia kufanya ziara nchini Sweden leo Jumatatu ambapo atakutana na mawaziri wakuu wa Sweden, Finland, Iceland na Norway.

https://p.dw.com/p/4fn2J
Kansela wa Ujerumani, Olaf Sholz
Kansela wa Ujerumani, Olaf Sholz.Picha: Hannes P. Albert/dpa/picture alliance

Agenda kuu za majadiliano ya viongozi hao zinatarajiwa kuwa hali ya usalama barani Ulaya, msaada kwa ajili ya Ukraine katika ulinzi wake dhidi ya Urusi, pamoja na kile kinachojulikana kama "vitisho vya mseto" kama vile mashambulizi ya mtandao na hujuma.

Aidha viongozi hao wanatarajia kutembelea kampuni ya teknolojia ya Ericsson ya Sweden kabla ya mkutano na waandishi wa habari baadae jioni.

Scholz anatarajiwa kuendelea na ziara yake nchini Sweden kesho Jumanne na anapanga kukutana na Waziri Mkuu Ulf Kristersson.