Ujerumani kuchunguza udukuzi wa Urusi kwa Bundeswehr
2 Machi 2024Akizungumza wakati wa ziara yake Vatikani, Scholz ameitaja kadhia hiyo kuwa suala zito. Mazungumzo hayo kati ya maafisa wa ulinzi wa Ujerumani yalichapishwa Ijumaa na mkuu wa shirika la utangazaji la Urusi, RT, Margarita Simonyan.
Ndani yake, maafisa wandamizi wa jeshi la anga wanajadili uwezekano wa kinadharia wa kupeleka makombora ya Ujerumani aina ya Taurus nchini Ukraine.
Scholz alikataa mara kwa mara kupeleka makombora hayo, licha ya maombi ya marakwa mara ya Ukraine, akisema anahofia kuitumbukiza Ujerumani zaidi katika vita vilivyoanzishwa na Urusi Februari 2022.
Soma pia:Ujerumani yawa mwenyeji wa mazungumzo ya amani kati ya Armenia na Azerbaijan
Sauti hiyo pia inahusisha mazungumzo nyeti ya kidiplomasia kuhusu Uingereza kuwa na watu wachache ndani ya Ukraine, kuhusiana na upelekaji wa makombora yake ya Storm Shadow nchini humo.