Schäuble aagwa katika bunge la Ujerumani
22 Januari 2024Matangazo
Karibu watu 1,500 walishiriki kwenye hafla hiyo iliyoandaliwa kwenye majengo ya bunge la Ujerumani, akiwamo Rais Emmanuel Macron, ambaye pia alisoma wasifu wake.
Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani, Rais wa Shirikisho Frank-Walter Steinmeier na Rais wa Bunge la Ujerumani, Bärbel Bas, pia wanahudhuria shughuli hiyo.
Schäuble aliyenusurika katika jaribio la kuuawa mwaka 1990, aidha alikuwa mbunge wa chama cha kihafidhina cha Christian Democrat kuanzia mwaka 1972 hadi kifo chake.
Tukio hili lilitanguliwa na misa katika Kanisa Kuu la Berlin Cathedral mchana wa Jumatatu (Januari 22).