Sauti ya usawa: Desmond Tutu atimiza miaka 90
Askofu wa kwanza mweusi wa Kianglikana wa Johannesburg, na baadaye akawa askofu mkuu wa Cape Town. Pamoja na Nelson Mandela, alipigana na ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.
Kuzeeka kwa neema
Tutu alizaliwa 1931 katika mji wa madini wa Klerksdorp. Alikua mwalimu. Wakati utawala wa ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini ulipoanza kubagua wanafunzi Weusi, Tutu alijiuzulu wadhifa wake. Alifuata taaluma ya theolojia na kuwa askofu mweusi wa kwanza wa Johannesburg. Hapa, Tutu alisherehekea miaka 86 ya kuzaliwa kwake. Anaunga mkono "Haki ya Kufa",ambayo ingeruhusu watu kuchagua kufa kwa heshima.
Mshirika wa Mandela
Kihistoria, Waafrika Kusini wengi humuweka Tutu katika hadhi sawa na Nelson Mandela, Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini aliyechaguliwa kidemokrasia na aliesimamia maoni ya kisiasa, wakati Tutu alisimamia maoni ya kiroho ya "Rainbow Nation", waangalizi wengi wanasema. Kwa wao, Afrika Kusini bila sauti ya Tutu haifikiriki.
Mbunifu wa Tume ya Ukweli na Maridhiano
Baada ya ubaguzi wa rangi kumalizika, Mandela alimuomba Tutu kuongoza Tume ya Ukweli na Maridhiano. Kusudi lake lilikuwa kwa wahasiriwa na wahalifu kukubali kuwa uhalifu ulifanywa wakati wa ubaguzi wa rangi. Tutu na TRC walijaribu kutafuta uuwiano wa haki ya mshindi, msamaha na upatanishi. Watu 2 000 walishiriki, na Tutu binafsi alihudhuria 1 500.
Tuzo ya Amani ya Nobel kwa kupambana na ubaguzi wa rangi
Upinzani usio na vurugu wa Desmond Tutu dhidi ya ubaguzi wa rangi unatambuliwa. Wakati Mandela na wapiganiaji wengine wa uhuru wakiteseka gerezani, Tutu alichukua vita dhidi ya ubaguzi wa rangi. Mnamo 1984 alipewa Tuzo ya Amani ya Nobel. Hapa, Egil Aarvik, mwenyekiti wa Kamati ya Nobel huko Oslo akimkabidhi tuzo hiyo.
Mnara hai
Mnamo 2005, mnara wa heshima wa washindi wa Tuzo ya Amani ya Afrika Kusini uliwekwa katika Uwanja wa Nobel wa Bandari ya Cape Town. Mchongaji-sanamu Claudette Schreuders aliwachonga watu hao wanne: Albert Luthuli (1960), Desmond Tutu (1984), F.W. de Klerk na Nelson Mandela, ambao walishiriki Tuzo ya Amani ya Nobel ya mwaka 1993.
Kiongozi wa kiroho mwenye uhusiano wa kimataifa
Askofu Mkuu Desmond Tutu, anayeitwa kwa upendo "Arch", amekua kiongozi wa maadili wa Afrika Kusini anaesimamia haki za binadamu na anapinga ubaguzi wa aina yeyote. Anajulikana kwa ucheshi wake, Tutu anachukuliwa kuwa hazina ya ulimwengu. Hapa anakutana na Dalai Lama, kiongozi wa kiroho wa Tibet, kwenye Mkutano wa Amani wa 2006 huko Hiroshima.
Tutu kwenye jukwaa la ulimwengu
Wakati Afrika Kusini ilishiriki Kombe la Dunia la FIFA mnamo 2010, Tutu hakukaa pembeni, alijionyesha kama mzalendo wa Afrika Kusini. Hapa yuko kamili Bafana Bafana (kama timu ya kitaifa ya mpira wa miguu ya Afrika Kusini inajulikana) kwenye mechi ya ufunguzi wa mashindano kati ya Afrika Kusini na Mexico. Kinachokosekana ni vuvuzela, Kifaa pendwa cha mashabiki katika viwanja vya Afrika Kusini.
Mwenye mamlaka ya maadili
Nelson Mandela alimjumuisha Desmond Tutu mapema katika jukwaa lake la "Wazee", ambalo alianzisha mnamo 2010. Shirika hilo, ambalo lilitafuta ushirikiano wa kimataifa katika suala la ubinadamu na haki za binadamu, linaweza kutegemea msaada wa hali ya juu kutoka kwa haiba ya kimataifa.
Tutu, mtu wa familia
Mke wa Desmond Tutu, Leah Nomalizo Tutu, alisimama pamoja naye wakati wote wa ubaguzi wa rangi. Mwenyewe alikuwa mwanaharakati, aliolewa na Tutu mnamo Julai, 1955 - kabla ya Tutu kubadilika kutoka katika kufundisha hadi kuhubiri. Wanandoa hao walipata watoto wanne na wajukuu tisa. Pamoja, walianza msingi wa kutetea utatuzi wa mizozo. Hongera kwako, "Arch" Tutu!