SiasaSudan
Saudi Arabia yatangaza mkutano wa kuichangia Sudan
14 Juni 2023Matangazo
Likunukuu wizara ya mambo ya kigeni shirika rasmi la Saudi Arabia limesema mkutano huo wa ahadi utafanyika Juni 19, na kuongeza kuwa utaongozwa kwa pamoja na Qatar, Misri, Ujerumani na Umoja wa Ulaya, pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa takribani watu milioni 25 ikiwa ni zaidi ya idadi jumla ya watu wa taifa hilo wanauhitaji wa msaada na ulinzi, lakini mwishoni mwa Mei kulitolewa dola milioni 2.6 katika kukabiliana na shida hiyo ikiwa sawa na asilimia 13 tu.
Kwa zaidi ya majuma manane Saudi Arabia na Marekani zimekuwa katika juhudi za upatanishi kati ya mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan na makamu wake wa zamani Mohamed Hamdan Daglo ambaye anaongoza kikosi cha kijeshi cha dharura.