1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saratani yawakumba wengi Kenya

Angela Mdungu
30 Julai 2019

Taasisi ya Kitaifa ya Saratani nchini Kenya imesema kuwa tezi dume na saratani ya koo zimewakumba watu wengi katika majimbo 11 yaliyofanyiwa utafiti nchini humo

https://p.dw.com/p/3MyMp
USA Blutproben
Picha: picture alliance/AP Photo/E. Thompson

Ripoti iliyowasilishwa kwa kamati ya bunge kuhusu afya na afisa mkuu mtendaji wa taasisi ya kitaifa ya saratani Alfred Kamau imefichua aina tatu kuu ya saratani zinazowakumba watu katika majimbo yaliyochaguliwa. Saratani hizo ni pamoja na tezi dume, saratani ya matiti na koo. Majimbo 11 yaliyochaguliwa yana viwango vya juu vya saratani. Majimbo hayo ni pamoja na Nairobi, Kisumu, Meru, Mombasa, Kakamega, Kiambu, Nyeri, Nakuru, Bomet, Embu and Eldoret.

Saratani ya koo imetajwa kuongoza kwa vifo katika majimbo ya Kisumu, Kakamega, Nyeri, Nakuru, Bomet na Eldoret. Kwa mujibu wa Taasisi hiyo, wanaume na wanawake ni waathiriwa.

Ripoti hiyo inaonesha kuwa wanaume wanaoishi katika majimbo ya Nairobi, Kiambu, Mombasa, Meru na Embu wana uwezekano mkubwa wa kukabiliwa na tezi dume. David Njoroge ni mwathiriwa wa ugonjwa huo.

Katika jimbo la Mombasa, wanaume wengi wanaugua tezi dume, huku wanawake wengi wakiugua saratani ya shingo ya kizazi. Taifa linapoendelea kukabiliana na athari za ugonjwa huu, pendekezo la kuanzisha sera ya kukabiliana nao, haijapitishwa bungeni. Kila mwaka taifa huandikisha visa vipya 47800 vya ugonjwa huo huku watu 32000 wakifariki dunia.

Ripoti hiyo inajiri wakati ripoti nyingine ikionesha kuwa wabunge 66 magavana watatu wanaugua ugonjwa huo. Kwa kipindi cha mwezi mmoja taifa limempoteza gavana mmoja, gavana wa kaunti ya Bomet, Dakta Joyce Laboso, na mbunge wa Kibra, Ken Okoth, kutokana na saratani.

Mwandishi: Shisia Wasilwa, Nairobi