1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sarah Obama afariki akiwa na umri wa miaka 99

29 Machi 2021

Sarah Obama, bibi yake aliyekuwa Rais wa 44 wa Marekani, Baraka Hussein Obama ameiaga dunia mapema asubuhi ya leo akiwa anapokea matibabu katika hospitali kuu eneo la Nyanza huko Kisumu eneo la Magharibi mwa Kenya.

https://p.dw.com/p/3rLHD
Afrika Obama besucht Kenia
Picha: picture alliance/landov/P. Souza

Kwa mujibu wa mmoja wa waandalizi wa mazishi ya Mama Sarah Obama, kiongozi wa Waislamu eneo la Kisumu Sheikh Musa Ismail Hajj, Bibi Sarah Obama aliyekuwa anapokea matibabu katika hospitali ya mafunzo na rufaa ya Russia iliyopo mjini Kisumu alifariki akiwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi mapema leo majira ya alfajiri baada ya kuugua kwa muda. soma zaidi Sarah Obama amsubiri mjukuu wake Barack

Sheikh Hajji anasema Mama Sarah Obama ambaye ameiaga dunia akiwa na miaka 99 alistahili kuzikwa leo kwa mujibu wa kanuni za dini ya Kiislamu ila, kufuatia makubaliano kati ya wanafamilia na kamati andalizi ya mazishi atazikwa kesho kabla ya swala ya Adhuhuri nyumbani kwake Kogello. Soma Zaidi  Rais Obama atatembelea Kogelo?

"Kwa niaba ya Waislamu Kisumu, kwa niaba ya familia tunasikitika kupoteza Mama yetu Nyanya yetu Mama Saraha Obama." amesema Sheikh Hajji.

Kenia USA Fotoreportage von Kogelo Dorf von Obamas Vorfahren
Picha: Reuters/T. Mukoya

Sababu ya kifo chake

Kadhalika, Sheikh Musa ambaye hajaelezea kikamilifu ni ugonjwa upi aliokuwa anaugua Mama Sarah Obama amesisitiza kuwa, Mama huyo hakuwa anaugua ugonjwa wa Covid 19.

"Mama alikuwa mgonjwa na ugonjwa kama magonjwa mengine ya kawaida, hajafariki na covid ." amesisitiza Sheikh Hajji.

Viongozi mbali mbali wameendelea kutoa rambi tambi zao kupitia mitandao ya kijamii kufuatia kifo cha Mama Sarah huku gavana wa Kisumu Prof. Peter Anyang Nyong'o aliyezuru hospitali ya Russia kuutizama mwili, amewasilisha rambi rambi za rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga akisema watasimama na wakaazi wa Kogello na familia kwa kifo cha mama huyo akisema mama huyo ameiacha historia kubwa.

Afrika Kenia Sarah Obama Porträt
Picha: Peter Macdiarmid/Getty Images

Alitambulika vipi?

"Leo ni siku ya huzuni kwa sababu tumempoteza mama yetu." amesema Anyang Nyong'o

Mama Sarah Obama, alitambulika na wengi nchini na hata duniani kutokana na Mjukuu wake Baraka Hussein Obama aliposhikilia wadhifa na seneta wa jimbo la Illnois Marekani na baadae akawa rais wa 44 wa Marekani na rais wa kwanza mweusi wa taifa hilo na kwa mara ya mwisho wawili hao kukutana ni wakati Obama alipokuwa nchini Kenya Julai mwaka 2018 akifika Kogello kuhudhuria ufunguzi wa kituo cha Sauti Kuu, mradi wa dadake Auma Obama. Soma Zaidi Kijiji cha Kogelo changoja kuwasili kwa Obama

Tayari mwili wa Mamam Sarah upo njiani kuelekea Kogello - Siaya.