SAO PAULO: Watu 200 wafariki Brazil katika ajali ya ndege
18 Julai 2007Matangazo
Ndege ya abiria ya Brazil imepata ajali baada ya kutereza kwenye njia ya kutua,katika uwanja wa ndege wa Congonhas.Inaaminiwa kuwa wote waliokuwemo ndani ya ndege hiyo wamepoteza maisha yao.Ndege hiyo aina ya Airbus A320,iligonga kizuizi cha uwanja wa ndege na ikaingia kwenye barabara kuu iliyojaa magari,kabla ya kusimama kwenye stesheni ya petroli na kushika moto.Kwa mujibu wa ripoti zisizothibitishwa,kama watu 200 wamefariki katika ajali hiyo.Ndege hiyo ya shirika la TAM la Brazil ilitokea Porto Alegre, kusini mwa Brazil.Inadhaniwa kuwa hali mbaya ya hewa huenda ikawa ndio ilisababisha ajali hiyo. Shirika la Airbus la Ulaya linalotengeneza ndege, limepeleka Brazil wataalamu wake 5 kusaidia kuchunguza ajali hiyo.