1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SAO PAULO: Papa Benedikti wa 16 atangaza mtakatifu Brazil:

12 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC33

Kiasi watu milioni moja walijumuika mjini Sao Paulo kumshuhudia kiongozi wa kanisa katoliki Papa Benedikti wa kumi na sita akimtangaza mtakatifu wa kwanza wa kanisa hilo mwenye asili ya Brazil.

Mtu huyo, Friar Antonio Galvao aliyeishi baina ya mwaka 1739 na mwaka1822 anasifika kwa kuanzisha nyumba za watawa na pia uwezo wake wa uponyaji.

Baadaye kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki aliwaambia maaskofu kiasi mia nne wa Brazil kwamba kanisa linakabiliwa na changamoto kuu kutokana na wafuasi wake kulihama na kujiunga na madhehebu mengine ya kikristo na hata wengine kupuuza imani ya Mungu.

Papa Benedikti alikariri msimamo wake kuhusu utoaji mimba akisema ni uhalifu dhidi ya maisha.

Papa alilalamika kwamba kanisa limeyaridhia mambo mengi ya wabunge kwa visingizio vya kuheshimu uhuru na haki ya mtu binafsi.