1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sao Paulo, Brazil. Pope awaasa vijana kuacha mambo yasiyofaa.

11 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3A

Kiongozi wa kanisa Katoliki Pope Benedict wa 16 ambaye yuko ziarani katika eneo la Amerika ya kusini amewaambia vijana wa Kikatoliki katika uwanja wa mpira wa mjini Sao Paulo kujizuwia na mambo mabaya kama madawa ya kulevywa, rushwa na uharibifu wa misitu ya Amazon.

Katika kile ambacho ni kuhimiza kampeni ya kupambana na ugonjwa wa ukimwi bila kutaja kwa hakika, amewataka vijana wajizuwie na ngono ama kufanya ngono kwa uangalifu ndani na nje ya ndoa.

Mapema jana Alhamis , Pope Benedict alikutana na rais Luiz Inacio Lula da Silva na kusema kuwa wasichana wapatapo mimba wakiwa wadogo , wanajipotezea nafasi za kuhudhuria masomo.

Akiwasili siku ya Jumatano , Pope alishutumu utoaji mimba na kusema kuwa anaunga mkono maaskofu wa Mexico ambao wametishia kuwatenga na kanisa wabunge wote ambao wamepiga kura mwezi uliopita kuondoa sheria ya kupiga marufuku utoaji mimba nchini humo. Mjini Sao Paulo mashoga na wanawake wa Kikatoliki wenye mtazamo wa kujiamulia mambo wameshutumu uongozi wa Pope kwa kuingilia mambo ya sera za kijamii za serikali ya Brazil.