SANTIAGO,Mahakama ya Chile kuamua juu ya kumkabidhi Fujimori kwa Peru
12 Julai 2007Matangazo
Mahakama kuu ya Chile itatoa uamuzi wake juu ya kumkabidhi kwa nchi yake aliyekuwa rais wa Peru Alberto Fujimori anayekabiliwa na mashtaka ya ulaji rushwa na ukiukaji wa haki za binadamu.
Hatua ya mahakama inakuja baada ya Peru kuapa kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa jaji wa kupinga kushtakiwa kwa rais huyo wa zamani wa Peru kutokana na matumizi mabaya ya mamlaka wakati wa utawala wake.
Waziri wa sheria wa Peru Maria Zavala amesema nchi yake imeshangazwa na uamuzi wa jaji Orlando Alvarez wa Chile.
Fujimori mwenye umri wa miaka 68 amekuwa kwenye kifungo cha ndani ya nyumba mjini Santiago Chile tangu mwaka 2005.