1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sakata la uraia wa mwanachama wa chama cha CCM nchini Tanzania

18 Agosti 2010

Sakata la uraia linalomkabili aliyekuwa mwanachama wa chama tawala nchini Tanzania cha CCM, Hussein Bashe bado linaendelea kuleta utata baada ya Idara ya Uhamiaji kuthibitisha kwamba mhusika ni raia.

https://p.dw.com/p/OqZ8

Hata hivyo bado chama tawala kinang'ang'ania kwamba si raia. Bashe alivuliwa uanachama na nyadhifa zote chamani kwa hoja kwamba hakuwa raia wa Tanzanaia. Sakata hilo lilianza baada ya kuwasilishwa malalamiko dhidi yake muda mfupi baada ya kushinda kwa kishindo katika kura ya maoni ya kumpata mgombea wa ubunge wa CCM katika jimbo la Nzega katika uchaguzi wa Oktoba mwaka huu.Itakumbukwa kuwa mwaandishi habari maarufu nchini Tanzania,Jenerali Ulimwengu, aliyewahi kuwa mkuu wa Wilaya kwa wakati mmoja, pia alikumbwa na mkasa kama huo na kutakiwa kuomba upya uraia.Ili kupata picha kamili Halima Nyanza alizungumza naye hivi punde ili kuupata mtazamo wake.

Mwandishi: Thelma Mwadzaya

Mhariri: Mohamed Abdulrahman