1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saif Al Islam akamatwa Libya

20 Novemba 2011

Serikali ya mpito nchini Libya imeahidi kumhukumu kwa haki mwanawe Muammer Gaddafi Saif al Islam, ambaye amekamatwa na wanamgambo katika jangwa lililopo kusini mwa nchi hiyo baada ya wiki kadhaa akiwa amejificha

https://p.dw.com/p/13DoR
Saif Al Islam Gaddafi akisafirishwa kwenda mjini ZintanPicha: picture alliance/abaca

Luis Moreno Ocampo  Mwendesha   Mashtaka  Mkuu wa mahakama inayopambana  na uhalifu wa kivita iliopo The Hague Uholanzi, inayokuwa   inamsaka  Saif  kwa uhalifu dhidi ya binaadamu, amesema ataelekea nchini Libya katika wiki zinazokuja kujadili wapi na vipi Saif Al Islam atashtakiwa.

Luis Moreno Ocampo Konferenz Den Haag Libyen
Kiongozi wa mashtaka wa mahakama ya ICC Hague Uholanzi Luis Moreno-Ocampo.Picha: picture alliance/dpa

Hapo jana Saif alisafirishwa hadi katika mji uliokuwa ukidhibitiwa na waasi uliopo magharibi mwa Tripoli, Zintan, ambako waziri mkuu wa mpito Abdurrahim el Keib amesema sheria za kimataifa zitaheshimiwa.

Aliongeza hatahivyo kuwa watu wa Libya wanataka kesi dhidi ya Saif ifanyike nchini humo. Umoja wa Ulaya na shirika la kujihami NATO, zimetoa wito kwa viongozi wapya wa  Libya wa  kushirikiana na mahakama ya kimataifa.

Abdel-Rahim al-Kib
Waziri mkuu mpya wa mpito Libya, Abdel-Rahim al-Keib .Picha: picture-alliance/dpa

Kanda za video za televisheni zilimuonyesha Saif akiwa na majeraha ya mkononi. Alikamatwa karibu  na  mji uliopo jangwani,Obari,  akiwa na wapambe  wake kadhaa waliokuwa na  silaha.

Walibya wengi walimiminika katika barabra za nchihiyo walipopokea taarifa za kukamatwa kwa  Saif.

Mwandishi Maryam Abdalla/rtre, dpae, ape

Mhariri:Mtullya Abdu