1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Saied awasilisha fomu kuwania tena urais Tunisia

5 Agosti 2024

Rais Kais Saied wa Tunisia aliyejilimbikizia madaraka makubwa miaka miwili baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi wa mwaka 2019, leo amewasilisha fomu ya kugombea tena urais katika uchaguzi wa Oktoba 6.

https://p.dw.com/p/4j89p
Rais Kais Saied wa Tunisia.
Rais Kais Saied wa Tunisia.Picha: Chokri Mahjoub/ZUMA Wire/IMAGO

Saied, mwenye umri wa miaka 66, amewaambia waandishi habari mjini Tunis kwamba uamuzi wake wa kugombea urais ni sehemu ya kile alichokiita "vita vya ukombozi" kwa nia ya kuanzisha jamhuri mpya.

Wachambuzi wamesema wapinzani wa Saied wamekabiliwa na vikwazo katika azma yao ya kuwania urais huku baadhi wakitiwa gerezani au kufunguliwa mashtaka.

Soma zaidi: Afisa mwandamizi wa chama cha upinzani nchini Tunisia akamatwa

Kiongozi huyo hata hivyo, amekanusha madai kwamba serikali yake inakandamiza sauti za wakosoaji.

Hatua ya Saied kuwasilisha rasmi fomu ya kuwania urais imetokea siku mbili tu baada ya mkosoaji wake mkubwa, Abir Moussi, ambaye amekuwa gerezani tangu mwezi Oktoba pia kuwasilisha fomu ya kuwania urais.