SiasaMarekani
Safari za ndege zacheleweshwa Marekani
11 Januari 2023Matangazo
Kwa mujibu wa wavuti unaofuatilia safari za ndege wa FlightAware karibu safari 1,200 za ndege zilichleweshwa kabla saa moja asubuhi hivi leo za kuingia au kutoka Marekani.
Safari nyingi za ndege zimecheleweshwa katika pwani ya mashariki ya Marekani. Wakala huo umesema unafanya juhudi kurekebisha hitilafu katika mfumo wake wa usimamizi wa safari za ndege.
Ndege zote za biashara na jeshi zinatakiwa kuongozwa na mfumo huo katika safari zao.
Msemaji wa ikulu ya Marekani Karine Jean-Pierre amesema hakuna ushahidi wa shambulizi la mtandaoni na Rais Joe Biden amefahamishwa kinachoendelea.