1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timu za Afrika kuanza safari ya kuelekea Urusi 2018

9 Novemba 2015

Wakati ligi kuu za kandanda Ulaya zikienda mapumziko kwa ajili ya michuano ya kimataifa, Cote d'Ivoire na Ghana zitaanzisha kampeni zao za kushiriki katika Kombe la Dunia la FIFA kwa mara yao ya nne mfululizo

https://p.dw.com/p/1H2Q5
Elfenbeinküste Fußball Nationalmannschaft
Picha: I. Sanogo/AFP/Getty Images

Timu hizo zina mechi za ugenini dhidi ya wapinzani wanaoorodheshwa chini yao katika viwango vya FIFA, Liberia na Comoros.

Nigeria watafunga safari kumenyana na na Swaziland ambapo kocha Sunday Oliseh amewaita kikosini Alex Iwobi wa Arsenal na Kelechi Iheanacho wa Manchester City. Aidha mshambulizi wa muda mrefu Obafemi Martins pia amerejea kwenye timu baada ya Emmanuel Emenike kustaafu.

Afrika Kusini watachuana ugenini dhidi ya Angola waati Cameroon ambao wanashikilia rekodi ya Afrika ya kucheza mara saba katika Kombe la Dunia wakipambana na Niger. Benin watashuka dimbani dhidi ya Burkina Faso wakati Morocco ambao wamefuzu mara nne wakitoana jasho na Guinea ya Ikweta. Cote d'Ivoire ambayo itakosa huduma za Yaya Toure itapambana na Liberia. Michuano hiyo inachezwa kesho na Jumatano

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP/Reuters
Mhariri: Yusuf Saumu