SADDAM HUSSEIN AFICHUA PESA ZILIPO
29 Desemba 2003Matangazo
DUBAI: Rais mpinduliwa Saddam Hussein wa Iraq ameyaambia majeshi ya ushirikiano wapi alipozificha pesa zinazokadiriwa kuwa kama Dola 40 bilioni.Hayo ni kwa mujibu wa Iyad Allawi mjumbe mmojawapo wa Baraza Tawala la Iraq lililochaguliwa na Marekani.Magazeti ya kiarabu Asharq Al-Awsat na Al-Hayat yamemnukulu Allawi akisema kuwa Saddam Hussein aliekamatwa majuma mawili ya nyuma,ameanza kutoa habari kuhusu pesa za taifa la Iraq alizozipeleka nchi za ngámbo kwa kutumia majina ya makampuni ya bandia.Sasa Saddam Hussein anakhojiwa juu ya uhusiano wake na mashirika ya kigaidi.Kwa mujibu wa Allawi,Saddam Hussein ameyataja majina ya watu wanaojua kule kulipofichwa silaha zinazotumiwa kuvishambulia vikosi vya Marekani na washirika wake pamoja na Baraza Tawala la Iraq.Kwa mujibu wa Allawi idadi ya magaidi waliotoka nchi za nje na kufanya mashambulio nchini Iraq ni zaidi ya 5,000.