Rykjavik, Greenland. Wito watolewa kuwapo na fikra mpya kuhusu mapambano ya mabadiliko ya hali ya hewa.
17 Agosti 2005Mwanzoni mwa mazungumzo ya mabadiliko ya hali ya hewa nchini Greenland, Denmark imetoa wito wa kuwapo na fikra mpya, juu ya njia za kupambana na mabadiliko hayo duniani.
Mawaziri na maafisa kutoka mataifa kadha ikiwa ni pamoja na Marekani, China , India, Mexico na mataifa ya umoja wa Ulaya wanahudhuria katika juhudi za kutatua mzozo mkubwa wa mtengano wa kisera baada ya Marekani kujiondoa katika mkataba wa umoja wa mataifa wa Kyoto wa kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa mwaka 2001.
Makubaliano ya Kyoto yanaonekana kuwa ni hatua ya kwanza kuelekea kuzuwia kupanda kwa hali ya joto duniani kutokana na gesi inayotokana na mafuta inayotoka katika vinu vya nishati, viwanda na magari.
Denmark inamatumaini kuwa mkutano huo wa Greenland utasaidia kutayarisha mazungumzo ya umoja wa mataifa nchini Canada mwishoni mwa mwezi Novemba.