1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda yapokea wakimbizi kutoka nchini Libya

27 Septemba 2019

Kundi la kwanza la wakimbizi 66 waliopokelewa kutoka Libya lawasili Kigali. Ni wakimbizi wa kiafrika waliokuwa wakishikiliwa kwenye vituo vya kuzuia wakimbizi vya Libya. Rwanda imesema iko tayari kupokea wakimbizi zaidi walioshindwa kufika Ulaya na kuishia kwenye vituo vya Libya vinavyodaiwa kuhusika katika vitendo vya kuwanyanyasa kingono,na kuwatesa wakimbizi wakiafrika.

https://p.dw.com/p/3QMyD