Rwanda imekubali kuwachukua mamia ya wakimbizi waliokwama Libya. Safari ya kwanza inayotarajiwa kuanza katika kipindi cha wiki chache toka sasa itawahusu wakimbizi takribani 500 kati ya wakimbizi 4,700 ambao wanahifadhiwa Libya. Hatua hiyo imefikiwa baada ya makubaliano ya Umoja wa Afrika na serikali ya Rwanda. Sikiliza mahojiano ya Sudi Mnette na mtaalamu wa masuala ya ukimbizi Robert Mkosamali.