1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda na Burundi zajumuishwa rasmi katika jumuiya ya Afrika Mashariki

18 Juni 2007

Viongozi kutoka jumuiya ya Afrika Mashariki wamekutana mjini Kampala Uganda kuzijumuisha rasmi Rwanda na Burundi kwenye jumuiya hiyo. Marais wa nchi wanachama wamezindua rasmi wimbo wa jumuiya ya Afrika Mashariki na kushuhudia kuapishwa kwa Julius Tangus Rotich raia wa Kenya kuwa naibu mpya wa katibu mkuu wa jumuiya hiyo. Aidha rais Yoweri Museveni wa Uganda amechukua wadhifa wa uenyekiti wa jumuiya hiyo kutoka kwa rais Mwai Kibaki wa Kenya.

https://p.dw.com/p/CB3W
Mwenyekiti mpya wa jumuiya ya Afrika Mashariki rais Yoweri Museveni wa Uganda
Mwenyekiti mpya wa jumuiya ya Afrika Mashariki rais Yoweri Museveni wa UgandaPicha: AP
Sikiliza mahojiano baina ya Thelma Mwadzaya na Juma Mapachu, katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki.