1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waasi wa M23 wauteka mji muhimu mashariki mwa DRC

29 Juni 2024

Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wameuteka mji wa kimkakati wa Kanyabayonga uliopo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4hfLT
DR Congo Kibumba 2022 | waasi wa M23
Waasi wa M23 na silaha zao huko Kibumba, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Desemba 23, 2022.Picha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Afisa mmoja ambae alizungumza kwa masharti ya kutotaka kutajwa jina lake alisema mji huo umekuwa katika udhibiti wa M23 tangu Ijumaa jioni. Kanyabayonga upo upande wa kaskazini mwa jimbo la Kivu Kaskazini, ambalo limekumbwa na ghasia tangu 2021, wakati ambapo waasi wa M23 walianzisha tena harakati zao katika eneo hilo.

Mji huo upo katika ulekeo wa maeneo muhimu ya kibiashara kati ya Butembo na Beni kaskazini. Ni makazi ya zaidi ya watu 60,000 pamoja na kuna maelfu ya waliokimbia makazi yao kutokana na kuongezeka kwa vurugu za uasi.

Mji huo ambao upo katika eneo la Lubero, unakuwa wa nne kudhibitiwa katika jimbo la Kivu Kaskazini baada ya mingine ya Rutshuru, Nyiragongo na Masisi.